Real Madrid Wanamtupia Jicho Nyota wa United Garnacho

Klabu ya Real Madrid ya nchini Uhispania wanafikiria kumnunua nyota wa Manchester United Alejandro Garnacho, ambaye ana umri wa miaka 18.

 

Real Madrid Wanamtupia Jicho Nyota wa United Garnacho

Mchezaji huyo alifanikiwa kuingia katika kikosi cha kwanza cha Manchester United kabla ya Kombe la Dunia, akifunga bao lake la kwanza kwa klabu hiyo katika ushindi wa 2-1 dakika za lala salama dhidi ya Fulham.

Gazeti la Uhispania Revelo linapendekeza Muargentina huyo amevutia macho ya Real Madrid, huku mabingwa hao wa Ulaya wakitaka kumuongeza kwenye safu ya ushambuliaji katika kikosi hicho.

Huku vijana wao kama vile Vinicius Junior, Rodrygo na Federico Valverde wakiwa tayari wameshamiri Bernabeu, wakuu wa Los Blancos wanaamini Garnacho anaweza kuwa nyota wao anayefuata.

Real Madrid Wanamtupia Jicho Nyota wa United Garnacho

Mkataba wa sasa wa winga huyo unamalizika msimu ujao wa joto na United tayari iko kwenye mazungumzo ya kuongeza mkataba wa mchezaji huyo. Alizaliwa katika mji mkuu wa Uhispania na alikaa miaka mitano Atletico Madrid kabla ya kuhamia Old Trafford mnamo 2020.

Real Madrid wamekuwa na shughuli nyingi katika kusaka watarajiwa wa kusisimua wa siku zijazo, huku Fabrizio Romano akiripoti kuwa dili la kumsajili kinda mshuhuri wa Brazil, Endrick limekubaliwa kwa mdomo.

Real Madrid Wanamtupia Jicho Nyota wa United Garnacho

Marca wanasema klabu hiyo imeamua kutomnunua mshambuliaji wa AC Milan Rafael Leao au nyota wa PSV Eindhoven Cody Gakpo, ambapo hilo litaipa United nguvu ya kumpata nyota wa Uholanzi Gakpo, 23, ambaye ndiye anayelengwa zaidi baada ya kampeni nzuri ya Kombe la Dunia.

Acha ujumbe