Mchezaji wa Chelsea Reece James ambaye anacheza katika nafasi ya beki wa kulia amezungumzia kuhusu jeraha lake na amesema kuwa anajaribu kuwa chanya, vilevile hajajua uhakika wa kupona utakuwa lini.

 

Reece James: "Sijajua Jeraha Langu Litapona Lini."

Reece ambaye amekosekana kwenye michezo kadhaa kutokana na jeraha alilolipata kwenye mchezo dhidi ya AC Milan kwenye mchezo wa marudiano ambapo timu yake ilishinda kwa bao 2-0.

Beki huyo ameiambia The Sun kuwa; hana uchungu, lakini akijaribu kuharakisha inaweza kumletea hatari kidogo huku taarifa zikisema kuwa beki huyo pia anaweza kulikosa Kombe la Dunia ambalo linatarajiwa kupigwa mwezi ujao huko Qatar.

Reece James: "Sijajua Jeraha Langu Litapona Lini."

Reece ambaye siku si nyingi ametoka kutia kandarasi ya kumfanya asalie klabuni hapo kwa muda mrefu amekuwa na kiwango cha kuvutia sana hapo Darajani na amesema kuwa kila siku hufanya awezalo kuboresha kiwango chake na anatarajia kupona haraka iwezekanavyo

Chelsea leo watakuwa ni wageni wa Brighton ambapo utakuwa ni mchezo wa kwanza wa Graham Potter dhidi ya timu yake ya zamani.

Reece James: "Sijajua Jeraha Langu Litapona Lini."

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa