Klabu ya Simba leo hii itamkaribisha Dodoma Jiji kwenye mchezo wa Ligi kuu ya NBC ambapo ni mchezo wa tano kwa Simba na mchezo wa sita kwa mgeni na mchezo huo utapigwa katika uwanja wa Benjamin Mkapa saa 19:00.

Simba Kumkaribisha Dodoma Jiji

Wekundu  mpaka sasa ndani ya mechi zake nne wameshinda tatu na wametoa sare moja, wakati kwa upande wa Dodoma Jiji wameshinda mchezo mmoja, wakitoa sare mbili na kupoteza michezo miwili.

Kocha msaidizi wa Msimbazi Selemani Matola amesema kuwa wamejiandaa vizuri kupata ushindi lakini pia kusema baadhi ya wachezaji watakosekana kwenye mchezo huo ambao ni Pape Sakho kutokana na matatizo ya kifamilia, Shomari Kapombe pamoja na Banda, na nahodha msaidizi wa timu hiyo Mohamed Hussein amesema kuwa wako tayari kufanya vizuri.

Simba Kumkaribisha Dodoma Jiji

Pia Dodoma Jiji nao kupitia kocha msaidizi wao wamesema kuwa watahakikisha wanashindana ili wapate ushindi mwingine wa pili kwenye ligi kuu ya NBC baada ya kupata alama zao za kwanza mchezo uliopita.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa