Kiungo wa muda mrefu wa klabu ya Athletico Madrid Koke anatarajiwa kuweka rekodi leo katika mchezo kati ya klabu yake na Sevilla katika dimba la Ramon Sanchez pizjuan.
Koke ataweka rekodi ya kucheza mechi nyingi zaidi klabuni hapo akiwapiku baadhi ya magwiji wa klabu hiyo kwa kuitumikia klabu hiyo kama gwiji Adelardo Rodriguez ambae nae alikua ana michezo mingi klabuni hapo.
Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 30 anaingia kwenye vitabu vya kumbukumbu vya klabu hiyo kama gwiji aliowahi kuitumikia klabu hiyo kwa mafanikio makubwa na kubaki na rekodi kama mchezaji alieitumikia michezo mingi klabu hiyo.
Wachezaji wanaomfuatia mchezaji huyo ni kama Pedro Thomas michezo (483) Enrique Collar (468) na Carlos Aguilera (456) lakini mpaka sasa Koke anakua kinara kwa kuitumikia klabu kwa jumla ya michezo 554.
Kiungo huyo ambaye ameibuliwa na shule ya vijana ya klabu hiyo na mchezo wake wa kwanza aliitumikia klabu hiyo dhidi ya klabu ya Barcelona ambapo walifungwa mabao 5 kwa mawili mwaka 2009.
Katika miaka 13 ambayo kiungo huyo ameitumikia klabu hiyo amefanikiwa kushinda mataji manane makubwa ikiwemo kombe la La Liga mara mbili mwaka 2014,2021 huku akifanikiwa kucheza fainali mbili za ligi ya mabingwa dhidi ya mahasimu wao Real Madrid.