Koke: Atletico Madrid Hatuiogopi Man City!

Nahodha wa Atletico Madrid, Koke anaamini timu yake haina jambo la kuogopa dhidi ya Manchester City kuelekea Robo Fainali za Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Atletico walijihakikishia nafasi yao kwenye robo fainali baada ya kuwalaza Man United kwa jumla ya Magoli 2-1.

Kwa mujibu wa staa huyu, Atletico walifanya vizuri mechi zote dhidi ya United, hivyo wamestahili kuwepo kwenye nafasi hiyo na wataitendea haki.

Hata hivyo, baada ya droo ya robo fainali, vijana wa Diego Simeone wanakutana na kibarua kizito zaidi cha kampeni yao ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya Manchester City.

Koke ana imani kuwa timu yake itafika nusu fainali.

“Itaenda kuwa mechi ngumu na mechi nzuri, itakuwa ni mara ya kwanza tunacheza dhidi ya Man City kwenye Ligi ya Mabingwa”

“Tumewachapa United, kwa nini tushindwe kuwachapa City? Tunaingia kwenye mechi hii tukiwa na hamasa ya hali ya juu, tulicheza vyema hatua iliyopita, na tunataka kufanya vuvyo hivyo kwenye robo fainali dhidi ya waliokuwa na nafasi kubwa ya kutwaa ubingwa mwaka 2021.” – Koke


SHAOLIN FORTUNES 100 ONJA LADHA YA USHINDI

Maana ya ushindi mkubwa ipo hapa katika mchezo wa SHAOLIN FORTUNES 100 ndani ya kasino maridhawa za meridianbettz. Kwa dau dogo unashinda zaidi, unaweza kucheza mara nyingi uwezavyo huku ukifurahia ladha ya ushindi.

liverpool, Liverpool Kila Mtu Ashinde Mechi Zake., Meridianbet

CHEZA HAPA

Acha ujumbe