Kocha wa klabu ya Tottenham Hotspurs Antonio Conte amekerwa na kitendo cha timu yake kupoteza mchezo katiika dimba la Emirates dhidi ya mahasimu klabu ya Arsenal.

antonio conteMchezo huo ambao umepigwa mapema leo katika dimba la Emirates na Spurs kupoteza kwa jumla ya mabao matatu kwa moja,magoli ya Thomas Partey,Gbariel Jesus,pamoja na Granit Xaka yalitosha kuwapa vinara hao wa ligi ushindi huku goli pekee la Tottenham likifungwa na Harry kane.

Baada ya vijana hao wa Antonio Conte kupoteza mchezo huo dhidi ya Arsenal unakua mchezo wa 12 wa klabu hiyo kutopata ushindi dhidi ya Arsenal katika dimba la Emirates baada ya kufungwa mechi 8 na kusuluhu michezo 4 huku ikiwa ni muda mrefu kidogo kwa Spurs kutokupata matokeo uwanjani hapo.

“Nadhani kipindi cha kwanza kilikua chenye usawa. Kipindi cha kwanza tulipata nafasi kadhaa za kufunga.Tulifanya makosa kwenye pasi ya mwisho na tulikua tuna nafasi kubwa ya kufunga mabao lakini hatukufanya hivo”.

“Kipindi cha pili tuliruhusu bao la mapema zaidi na tunaweza kufanya vizuri zaidi kwenye hali kama hii”. Baada ta kadi nyekundu mchezo uliondoka upande wetu,Tulijaribu kucheza kutoka nyuma lakini mchezo ukawa mgumu na kwa sifa za wachezaji wetu na sitaki kuongelea uamuzi wa mwamuzi”Alisema Antonio Conte.

Tottenham wanaendelea kua wateja wa Arsenal katika dimba la Emirates kitu kinachoifanya Spurs iendelee kuonekana dhaifu mbele ya Arsenal licha ya ubora wao.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa