Klabu ya Liverpool imeendelea kuapata matokeo ya kusuasua katika ligi kuu ya Uingereza baada ya kulazimishwa sare na klabu ya Brighton Hove Albion katika dimba lao la Nyumbani.
Klabu hiyo inaonekana kuanza ligi kwa mguu wa kushoto katika michuano mbalimbali msimu huu hasa katika ligi kuu ya Uingereza kutokana na matokeo ambayo wameyapata mpaka sasa katika ligi hiyo baada ya kushinda michezo 4 na kusuluhu michezo miwili na kufungwa mchezo mmoja na kuvuna jumla ya alama 10 mpaka sasa ambao ni wastani mdogo kwa klabu ya Liverpool.
Vijana wa Jurgen Klopp walitoka nyuma baada ya kuongozwa kwa mabao mawili na yaliyofungwa na Leandro Trossard huku magoli mawili ya kusawazisha ya Liverpool yakifungwa na Roberto Firmino kabla ya mchezaji wa Brighton Webster kujifunga na kuwapa uongozi majogoo huku dakika za lala salama Leandro Trossard kusawazisha na matokeo kuisha kwa sara ya magoli matatu kwa matatu.
Klabu hiyo ambayo imekua ikifanya vizuri kwa takribani miaka minne sasa imeanza msimu vibaya sana huku ikiwa imeruhusu idadi kubwa ya magoli tofauti na misimu kadhaa nyuma.