Alcaraz Ajiondoa Davis Cup Baada ya Kutwaa Taji la US Open

Nyota wa tenisi kutoka Hispania, Carlos Alcaraz, ametangaza kujiondoa katika mashindano ya kufuzu Davis Cup dhidi ya Denmark wiki hii, licha ya kujumuishwa awali kwenye kikosi cha taifa.

Uamuzi huo unakuja siku chache baada ya Alcaraz kuibuka kidedea kwenye fainali ya US Open, akimshinda mpinzani wake wa muda mrefu, Jannik Sinner, kwa mchezo wa kipekee uliompa taji lake la sita la Grand Slam.

Alcaraz Ajiondoa Davis Cup Baada ya Kutwaa Taji la US Open

Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Hispania, ikiwemo Cadena SER, Alcaraz ameamua kujipa mapumziko kutokana na uchovu na uhitaji wa kupata muda nje ya korti. Nafasi yake kwenye kikosi cha Hispania sasa itachukuliwa na Jaume Munar.

Hali ya kikosi cha Hispania imezidi kuwa na changamoto baada ya kuibuka wasiwasi juu ya jeraha la mguu kwa mchezaji mkongwe Marcel Granollers (39), ambaye anatarajiwa kufanyiwa vipimo mjini Barcelona. Hali hii inamuweka nahodha David Ferrer kwenye mtihani mgumu wa kupanga safu ya timu.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

Alcaraz Ajiondoa Davis Cup Baada ya Kutwaa Taji la US Open

Licha ya kuachana na Davis Cup, Alcaraz bado anatarajiwa kushiriki kwenye Laver Cup, ambapo ataichezea Timu ya Ulaya sambamba na Holger Rune, Casper Ruud, Jakub Mensik, Alexander Zverev na Flavio Cobolli. Baada ya hapo, atashiriki kwenye China Open, Shanghai Masters, Paris Masters, kabla ya kuhitimisha msimu kwenye ATP Finals.

Wakati mashabiki wa tenisi wakimsubiria Laver Cup na safari yake kuelekea Melbourne mwakani, kijana huyu wa Hispania anaendelea kuthibitisha nafasi yake kama uso mpya wa tenisi duniani.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.