Soka la Afrika linaendelea kushika kasi huku hatua ya kufuzu Kombe la Dunia 2026 ikifikia Raundi ya 8. Timu kadhaa kubwa zipo uwanjani leo, zikisaka pointi muhimu zinazoweza kufungua milango ya kwenda Marekani, Mexico na Kanada mwakani. Baadhi ya michezo mikubw inayosubiri kutazamwa na wengi ni pamoja na;
Zambia dhidi ya Morocco.
Pambano la kufungua dimba ni la aina yake. Zambia wanakutana na timu bora barani Afrika, Morocco, waliowahi kucheza nusu fainali ya Kombe la Dunia 2022. Chipolopolo wanahitaji kushinda ili kusalia kwenye mbio, lakini Morocco wana kikosi kilichojaa nyota wa Ulaya huku wakiwa wamefuzu tayari.
Mozambique dhidi ya Botswana.
Mozambique wakiwa Maputo wanataka kuendeleza mwendo mzuri, lakini Botswana wameonyesha uimara katika mechi za hivi karibuni. Ni mchezo wa pointi tatu unaoweza kubadilisha nafasi za kati ya kundi. Huku mchezaji wa kuangaliwa kwa upande wa Mozambique akiwa ni Geny Catamo anayecheza Sporting Lisbon anayesifika kwa kuwa na kasi na uwezo wa kufunga.




