Yanga Yafungua Ukurasa Mpya, Mkutano Mkuu 2025

Klabu ya Yanga SC imeandika historia mpya katika safari yake ya ukuaji baada ya kufanikisha Mkutano Mkuu wa Wanachama (AGM) wa mwaka 2025, ambapo maamuzi na mipango mikubwa yamepitishwa kwa lengo la kuendeleza mafanikio ndani na nje ya uwanja.

Kwa mara ya kwanza, thamani ya Yanga imetangazwa kufikia shilingi 100 bilioni (takribani dola za Marekani milioni 38.5), ishara ya ukuaji wa kibiashara na ushawishi wa klabu hiyo katika soka la Afrika.

Yanga Yafungua Ukurasa Mpya, Mkutano Mkuu 2025

Wajumbe wa mkutano huo walipitisha bajeti ya shilingi bilioni 33 kwa msimu wa 2025/26 (takribani dola milioni 12.7). Bajeti hiyo inalenga kuimarisha kikosi, miradi ya maendeleo ya miundombinu na programu za kijamii zinazohusiana na klabu.

Msimu uliomalizika umetajwa kuwa wa mafanikio makubwa kwa Yanga, baada ya kutwaa makombe matano kati ya sita waliyoshindania. Mafanikio hayo yameifanya klabu kuendeleza rekodi yake kama moja ya timu zenye historia kubwa na mafanikio barani Afrika Mashariki.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

Yanga Yafungua Ukurasa Mpya, Mkutano Mkuu 2025

Habari kubwa zaidi iliyowafurahisha wanachama ni tangazo la kuanza ujenzi wa uwanja mpya wa kisasa wenye uwezo wa kuchukua mashabiki 20,000. Mradi huu unatarajiwa kuanza msimu huu, na unaonekana kuwa hatua muhimu katika kujenga urithi wa kudumu kwa Yanga na mashabiki wake.

Rais wa klabu, Eng. Hersi Said, ambaye pia ni Mwenyekiti wa African Clubs Association (ACA), alitumia nafasi hiyo kupongeza mshikamano wa wanachama na viongozi, akisisitiza kuwa mshikamanio huo ndio msingi wa mafanikio makubwa yaliyopatikana.

“Yanga siyo tu klabu ya soka, ni taasisi yenye malengo makubwa. Tutaendelea kukua ndani na nje ya uwanja,” alisema Hersi.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.