Yanga Wanaipigia Hesabu Kali Ngao Ya Jamii

Klabu ya Yanga imeanza mikakati kabambe ya kuhakikisha inapata ushindi katika mchezo wake wa Ngao ya Jamii dhidi ya watani zao wa jadi, Simba, unaotarajiwa kupigwa, Septemba 16, mwaka huu, Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.

Makamu wa Rais wa klabu hiyo, Arafat Haji, amesema kuwa mipango na mikakati ya mechi hiyo imeshaanza ambapo lengo ni kupata ushindi ili kuendelea kulihifadhi taji hilo. Alisema kuwa heshima ya Yanga kwa msimu wa 2025/26, itaanza kuwekwa katika mchezo huo.

Yanga Wanaipigia Hesabu Kali Ngao Ya Jamii

“Tuna kazi tarehe 16, jamaa walitamani ule mfumo ungeendelea, walitamani ungendelea kuchezwa kwa mfumo wa nusu fainali ili watukimbie tena, lakini wanasema Mungu si Athumani, kawaleta, siku hiyo tutaanza kuweka heshima ya Yanga kwa msimu wa 2025/26,” alisema Haji.

“Tutakwenda kuhakikisha Ngao ya Jamii inakwenda nyumbani, ibakie Jangwani kwa sababu ni kwao, hivyo ushirikiano wa Wanayanga wote ule uliooneshwa msimu uliopita uongezeke mara dufu msimu huu.”

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

Yanga Wanaipigia Hesabu Kali Ngao Ya Jamii

Hivi karibuni, Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), lilitangaza mabadiliko ya Kanuni ya Ligi Kuu msimu huu ambapo badala ya kucheza mechi tatu, nusu fainali mbili na fainali moja, kwa timu nne kushiriki, badala yake itacheza mechi moja tu.

Kwa mujibu wa TFF, mchezo huo utahusu bingwa wa Tanzania Bara ambaye ni Yanga, watakaocheza na mshindi wa pili wa Ligi Kuu, Simba. Timu hizo zitalazimika kucheza mechi hiyo kutokana na kanuni kwani Yanga ilibidi icheze na bingwa wa Kombe la FA, lakini kwa sababu yenyewe ndiye bingwa pia wa makombe yote mawili, hivyo kanuni inasema itacheza na mshindi wa pili wa Ligi Kuu.

TFF, ilifafanua kuwa mfumo wa mashindano hayo umebadilika msimu huu kutokana na marekebisho ya kanuni zilizopitishwa hivi karubuni na Kamati ya Utendaji ya TFF.

Moja ya marekebisho hayo yanasema ikitokea mazingira kama ya sasa ambapo mashindano yanayosimamiwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) yamebana ratiba za TFF, basi itachezwa mechi moja tu ya Ngao ya Jamii.

Yanga Wanaipigia Hesabu Kali Ngao Ya Jamii

Yanga imeifunga Simba mara tano mfululizo, mara nne kwenye mechi za Ligi Kuu kwa misimu miwili mfululizo, nyumbani na ugenini pamoja na mchezo mmoja wa nusu fainali ya Ngao ya Jamii uliochezwa, Agosti 8, mwaka jana.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.