Inter na Atletico Madrid wameungana kwa ajili ya mpango wa kupinga ubaguzi wa rangi We Love Football kabla ya mechi yao ya Ligi ya Mabingwa na ujumbe kutoka kwa Marcus Thuram. ‘Kandanda ni chuo kikuu cha maisha.’
Mechi ya mkondo wa kwanza wa hatua ya 16 bora itachezwa Jumanne huko San Siro.
Cha kusikitisha ni kwamba wiki chache zilizopita kuwakuwa na unyanyasaji zaidi wa kibaguzi unaolenga wachezaji sio tu na wapinzani, lakini hata kutoka kwa mashabiki wao ambao walikuwa wakikosoa makosa.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa.
Thuram alikaa na timu ya mitandao ya kijamii ya Atletico Madrid kutuma ujumbe kwa kila mtu kwamba soka ni mchezo ambao wote wanajisikia kukaribishwa.
“Kandanda ni mchezo kwangu, mchezo ambao nilikuwa nikiupenda nilipokuwa mtoto, nikiwa na ndoto ya kuwa mwanasoka,” alisema Thuram, ambaye baba yake Lilian alichezea Parma na Juventus.
Mchezaji huyo amesema kuwa, kufunga mabao, kunaleta furaha kwa watu wanaokuja kuwatazama uwanjani, ndio wanaowasaidia, mchezo baada ya mchezo. Kandanda ni chuo kikuu cha maisha, ambapo unakua na wachezaji wenzako, kwa heshima. Lazima ujifunze nini maana ya kazi ya pamoja.
Mitandao ya kijamii imeleta wachezaji karibu zaidi na wafuasi na kuonyesha upande tofauti kwao, lakini pia kuweka uwajibikaji zaidi mabegani mwao.
Wacheza kandanda ni “role model” wa watu wengi katika ulimwengu wa sasa. Wao ni mfano kwa watoto wengi na watu wazima, pia. Ikiwa kuna ujumbe ambao unahitaji kutumwa, wanasoka wanaweza kufanya hivyo kutokana na athari waliyo nayo kwa jamii.
“Kandanda inaweza kusaidia kuleta watu pamoja, kuwa na ndoto, kubadilisha maisha yako.” Alisema Thuram.