Casemiro Anaamini Brazil Inaweza Kustahimili Kumkosa Neymar

Casemiro ana imani kuwa Brazil inaweza kushinda bila Neymar kwa sasa kwani alimuunga mkono mchezaji huyo ili kuwa fiti kwa wakati kwa ajili  ya Kombe la Dunia.

 

Casemiro Anaamini Brazil Inaweza Kustahimili Kumkosa Neymar

Jeraha la kifundo cha mguu lilimlazimu Neymar kubadilishwa dakika ya mwisho katika ushindi wa 2-0 wa Brazil dhidi ya Serbia siku ya Alhamisi, huku wakiendeleza kampeni yao ya Qatar 2022.

Richarlison alifunga mabao yote mawili ya Brazil na kiwango cha mshambuliaji huyo wa Tottenham ni sababu moja inayompa moyo kiungo mkabaji Casemiro. Neymar bila shaka atakosa mchezo dhidi ya Uswizi hapo kesho na kuna uwezekano mkubwa wa pambano dhidi ya Cameroon siku ya Ijumaa.

Iwapo anaweza kupona kwa wakati ili kushiriki katika hatua ya mtoano bado haijajulikana lakini Brazil wana matumaini huku Casemiro akinukuliwa akisema kuwa;  “Ikiwa  tutaendelea kuzungumza kuhusu Neymar, tutakaa hapa kwa siku, kwa sababu ya umuhimu wake,  yeye ndiye nyota wa timu, ambaye analeta mabadiliko, lakini tuna wachezaji wengine kama kina Raphina Richarlison Viniciouz na wengine wengi.”

Casemiro Anaamini Brazil Inaweza Kustahimili Kumkosa Neymar

Neymar ni mmoja wa wachezaji bora zaidi Duniani, na kwa bahati mbaya hatakuwepo kwenye mchezo ujao lakini tuna wachezaji wenye ubora wa kuchukua nafasi yake, lakini bila shaka si katika kiwango chake.

Casemiro alimtaja Lucas Paqueta wa West Ham kama mchezaji ambaye anaweza kuingia kwenye kikosi cha kwanza na kuleta ufahamu zaidi iwapo Neymar hayupo.

Beki Danilo pia hayupo kwenye kikosi cha Brazil kwa sasa, lakini nyota wa Manchester United, Casemiro anawaunga mkono wote wawili ili kurejea kwenye kinyang’anyiro cha kuwania kikosi cha kwanza cha Tite.

Casemiro Anaamini Brazil Inaweza Kustahimili Kumkosa Neymar

“Danilo na Neymar wanafanya kazi asubuhi, mchana na usiku, wakifanya juhudi kubwa zaidi Duniani. Wanajua wao ni muhimu, tuna wataalamu wakubwa na afya ndio kwanza. Watafanya kila kitu kurudisha asilimia 100 haraka iwezekanavyo.”


Je wewe hucheza Kasino Mtandaoni na umekuwa ukijiuliza ni mchezo gani rahisi na mzuri kwa ushindi? Basi Usihangaike Aviator ni rahisi zaidi kucheza na kushinda, kingine cha zaidi ni kwamba Aviator Bonanza imerudi tena Cheza zaidi ujiweke kwenye nafasi ya kushinda Samsung A23.

BONYEZA HAPA KUCHEZA

 

 

HISPANIA

 

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.