Kocha wa Real Madrid Carlo Ancelotti anatarajia kuwa mlinda mlango wake Thibaut Courtois atarejea kutoka kwenye jeraha ambapo wanatarajia kucheza mechi yao ya Derby ya El Clasico dhidi ya Barcelona.

Madrid ilimpumzisha Courtois kwa kipindi kisichojulikana mwanzoni mwa mwezi walipogundua kuwa alikuwa na jeraha, ambapo hilo lilikuja muda mfupi baada ya dirisha la hivi majuzi la Kimataifa, kumaanisha kwamba Courtois hajaichezea Madrid tangu waliposhinda 2-1 dhidi ya Atletico Madrid mnamo Septemba 18.
Golikipa huyo amekosa mechi tatu katika mashindano yote na pia hatakuwepo leo katika mechi ya pili ya marudiano kati ya Real Madrid ikichuana na Shakhtar Donetsk kwenye ligi ya mabingwa ambapo Mechi ya kwanza Ancelotti alishinda kwa mabao 2-1.

Lakini kikubwa zaidi ni kwamba, kipa huyo ambae ni chaguo la kwanza la Ancelotti anatarajiwa kuwa tayari kwa mchuano wa Jumapili na Barca katika uwanja wa Santiago Bernabeu. “Courtois ni bora zaidi,” Ancelotti alisema Jumatatu.
Kocha huyo amesema kuwa mpango wake ni kwamba Courtois aanze mazoezi siku ya Alhamisi ili awe tayari kwa mechi ya Jumapili dhidi ya mahasimu wao wakubwa Barca. Wamezungumza nae na yupo vizuri.
Pia baada ya Karim Benzema kuumia kwenye mechi ya Celtic na kukosekana kwa wiki tatu akiwa nje ya uwanja baada ya kupata jeraha la paja atakuwepo hii leo kwenye mechi hiyo. Ancelotti alisema;

“Karim yuko sawa na ni wazi kuwa kesho anaanza, na Toni Kroos na Ferland Mendy, ambao wako safi na wataenda kucheza,”
Lakini Vinicius Junior, ambaye ameanza mechi zote 12 za Madrid katika mashindano yote msimu huu, anaweza kulazimika kupumzika, na aliongeza kwa kusema kuwa Vini ni kati ya wachezaji anaopaswa kuwatathmini kwasababu amecheza kila kitu kabla ya safari hii.

