Timu ya wanawake Simba Queens kutoka Tanzania imeweka rekodi ya kuwa timu ya kwanza kwa wanawake kufuzu hatua ya Nusu Fainal ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika baada ya kuitungua Green Buffaloes kwa mabao 2-0.

Mchezo huo ulipigwa katika uwanja wa Grand Stade De Marrakech majira ya saa 4:00 usiku huku mchezo huo ulikuwa muhimu sana kwa Simba Queens kupata matokeo hayo ili waweze kuvuka hatua inayofuata.
Kutinga kwa nusu fainali kwenye Ligi ya Mabingwa Simba watapata Milioni 400 za Kitanzania kutokana na kufuzu hatua hiyo, huku Opa Clement akichaguliwa kuwa mchezaji bora wa mchezo huo.

Mabao hayo mawili yalitupiwa kimyani na Asha Djafar katika dakika 64 na baadae Opa Clement akapachika bao la pili ambalo liliifanya Simba iongoze mpaka dakika 90 za mchezo kumalizika.
Timu hiyo ilianza safari yao kwa kupoteza mchezo wa kwanza kwa bao 1-0 dhidi ya mwenyeji Far Rabat, na mechi ya pili akashinda kwa mbao 2-0 dhidi ya Determine Girls ya Liberia na mechi ya jana ya kufuzu akashinda mabao mawili tena.

Kocha Mkuu wa Simba Queens Charles Lukula na Vijana wake sasa wanasubiria watapangwa na nani katika hatua hiyo ya nusu fainali huku wakiendelea kujiandaa na kujiweka vyema kwa mchezo huo unaofuata.

Ulishawahi kuwaza kuwa rubani wa maisha yako!! Kuwa rubani wa mchezo pendwa wa Aviator wa kasino mtandaoni. Aviator bonanza inazidi kutoa michongo ya mkwanja kwenye nyumba ya mabingwa. Unarusha ndege yako na unashinda, kuwa rubani wa kujivunia kwa kuibuka na mkwanja leo.
BONYEZA HAPA

