Klabu ya Atalanta imeshindwa kumzuia Napoli kukaa kileleni hapo jana baada ya kupigwa mabao 2-1 wakiwa nyumbani kwao na kuwafanya washuke hadi nafasi ya 3 wakiwa na pointi zao 27 kwenye msimamo.

 

Atalanta Yashindwa Kumzuia Napoli Nyumbani Kwake

Atalanta ndio waliotangulia kupata bao mapema kabisa la mkwaju wa penati kupitia kwa mchezaji wao Ademola Lookman na dakika ya 23 ya mchezo vijana wa Spalletti wakasawazisha bao hilo.

Lakini Napoli hawakuchelewa kupata bao la pili la kuongoza katika dakika ya 35 baada ya kuyatumia makosa ambayo Atalanta waliyafanya na kuwapekea kwenda mapumziko wageni wakiongoza kwa 2-1.

Atalanta Yashindwa Kumzuia Napoli Nyumbani Kwake

Ushindi huo wa jana umewafanya Naples kukaa kileleni huku wakiwa na malengo yao msimu huu ya kunyanyua taji la ligi hiyo wakiwa na wachezaji ambao wamekuwa bora sana msimu huu.

Licha ya Atalanta kuwa wenyeji wa mchezo lakini walizidiwa kupiga mashuti yaliyolenga lango pamoja na umiliki wa mpira huku wakizawadiwa adhabu za kadi za njano 5 peke yao huku Napoli akipata moja pekee.

Atalanta Yashindwa Kumzuia Napoli Nyumbani Kwake

Mechi inayofuata Atalanta atasafiri na kwenda kukipiga dhidi ya Lecce siku ya Alhamisi wakati Naples yeye atakuwa nyumbani kumkaribisha Empoli.


aviator

Ulishawahi kuwaza kuwa rubani wa maisha yako!! Kuwa rubani wa mchezo pendwa wa Aviator wa kasino mtandaoni. Aviator bonanza inazidi kutoa michongo ya mkwanja kwenye nyumba ya mabingwa. Unarusha ndege yako na unashinda, kuwa rubani wa kujivunia kwa kuibuka na mkwanja leo.

BONYEZA HAPA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa