Martinez Amesema Lukaku Amerejea Mazoezini

Kocha mkuu wa Ubelgiji Roberto Martinez amesema kuwa mshambuliaji wake Romelu Lukaku amerejea mazoezini lakini hakuna uwezekano wa mchezaji huyo kuanza kwenye mechi yao ya pili ya Kombe la Dunia watakapokipiga dhidi ya Morocco.

 

Martinez Amesema Lukaku Amerejea Mazoezini

 

Lukaku amecheza mechi tano pekee akiwa na Inter katika msimu ambao ulikuwa wa majeraha kwake na hakuwepo wakati Ubelgiji ikianza kampeni ya Kundi F kwa ushindi mgumu wa 1-0 dhidi ya Canada Jumatano.

Huku Martinez akitumaini kuwa mfungaji bora huyo wa muda wote wa Ubelgiji atarejea  dhidi ya Morocco kwenye Uga wa Al Thumama Jumapili, huku mshambuliaji huyo wa Nerazzurri  akilazimika kukaa benchi.

Martinez alisema kuwa; “Leo, alifanya mazoezi na kundi, sasa tutaona jinsi mwili wake utakavyofanya, sidhani kama yuko tayari kucheza na Morocco tangu mwanzo, lakini tutagundua hilo katika siku mbili zijazo.”

Martinez Amesema Lukaku Amerejea Mazoezini

Iwapo Ubelgiji itawashinda vijana wa Walid Regragui mara nyingine, watakuwa timu ya kwanza katika historia ya Kombe la Dunia kushinda mechi tisa mfululizo za makundi kwenye michuano hiyo.

Ubelgiji pia hawajapoteza katika mechi zao nne zilizopita za Kombe la Dunia na timu za Afrika ambapo walishinda mechi tatu, na sare moja, wakishinda Tunisia 5-2 katika mchuano wao wa mwisho kama huu mnamo 2018.

Martinez Amesema Lukaku Amerejea Mazoezini


Kombe la Dunia Linatimua Vumbi huko Qatar ni timu 32, sawa na mechi 64 zitapigwa kwenye viwanja tofauti. Meridianbet wana uwanja wao wa Kushiriki na wewe wakati Michuano hii inaendelea. Uwanja wa Machaguo Spesho ni Kwa ajili yako, wewe Bingwa wa Kubeti. Unaweza kubeti ni Timu gani itachukua Ubingwa, Timu gani Itaongoza kuwa na kadi nyingi za Njano na Nyekundu, au Timu gani itatoka mapema kwenye michuano hiyo. Uamuzi ni wako. Chaguo ni lako. Hii ipo mpaka mwisho wa Kombe la Dunia.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.