Tite: "Jeraha la Neymar Halitamfanya Asicheze Kombe la Dunia"

Kocha mkuu wa Brazil Tite ana imani kwamba Neymar ataendelea kucheza Kombe la Dunia licha ya jeraha la kifundo cha mguu alilopata kwenye mechi ya ufunguzi akiwa na Serbia hapo jana.

 

Tite: "Jeraha la Neymar Halitamfanya Asicheze Kombe la Dunia"

Mchezaji  huyo wa Paris Saint-Germain alitoka uwanjani kwa kuchechemea katika dakika za mwisho za ushindi wa 2-0 wa Brazil, ambapo mabao hayo ya ushindi yalifungwa na Richarlison kipindi cha pili na kumfanya Tite aondoke kifua mbele.

Neymar alionekana kutokwa na machozi alipokuwa akipata matibabu kwenye benchi, kabla ya kupigwa picha akiwa na kifundo cha mguu kilichovimba alipokuwa akielekea kwenye chumba cha kubadilishia nguo.

Daktari wa timu ya Brazil Rodrigo Lasmar alithibitisha kuwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 30 atafanyiwa uchunguzi zaidi kati ya saa 24 hadi 48 zijazo lakini Tite, aliweka wazi kuwa Neymar aliendelea kucheza dakika 11 zaidi baada ya kupata jeraha hilo, na anasisitiza kwamba atarejea.

Tite: "Jeraha la Neymar Halitamfanya Asicheze Kombe la Dunia"

Tite alisema kuwa; “Neymar alihisi maumivu haya muda wote wa mchezo, lakini aliamua kusalia uwanjani kusaidia timu yake na ni ajabu kwamba aliweza kuvumilia haya wakati timu yake inacheza.”

Kocha huyo wa Selecao amesema kuwa ana imani kwamba Neymar ataendelea kucheza Kombe la Dunia na hakuona kama mchezaji huyo wa PSG ameumia kiasi kwamba asiendelee na michuano hii kwani chenga aliyopiga ndiyo ilisababisha jeraha hilo.

Tite: "Jeraha la Neymar Halitamfanya Asicheze Kombe la Dunia"


Kombe la Dunia Linatimua Vumbi huko Qatar ni timu 32, sawa na mechi 64 zitapigwa kwenye viwanja tofauti. Meridianbet wana uwanja wao wa Kushiriki na wewe wakati Michuano hii inaendelea. Uwanja wa Machaguo Spesho ni Kwa ajili yako, wewe Bingwa wa Kubeti. Unaweza kubeti ni Timu gani itachukua Ubingwa, Timu gani Itaongoza kuwa na kadi nyingi za Njano na Nyekundu, au Timu gani itatoka mapema kwenye michuano hiyo. Uamuzi ni wako. Chaguo ni lako. Hii ipo mpaka mwisho wa Kombe la Dunia.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.