Kocha mkuu wa Brazil Tite amesifu  uchezaji “wa kuvutia” wa timu yake baada ya kuitungua timu ya Taifa ya Ghana mabao 3-0, ambapo mabao hayo yote yalifungwa katika kipindi cha kwanza cha mchezo.

 

Brazil Yamvutia Tite

Timu hiyo ya Amerika ya Kusini iliibuka na ushindi huo katika mechi ya kirafiki dhidi ya wapinzani wao kutoka Afrika ambapo mechi hiyo ilipigwa katika jiji la Ufaransa. Marquinhos aliiandikia Brazil bao la kwanza katika dakika ya 9 kabla ya Richarlison kupachika mabao mawili kabla ya mapumziko.

Ushindi huo unaongeza matumaini kwa Mabingwa hao mara tano wa kombe la Dunia  kabla ya michuano hii kuanza Novemba mwaka huu huko Qatar, huku kikosi cha Tite kikifanya vyema katika nafasi ya tatu ya mwisho na kuwafanya wapinzani wao wajitafakari kuelekea michuano hiyo.

 

Brazil Yamvutia Tite

Hata hivyo Tite alifurahishwa na jinsi ambavyo timu yake ilicheza kwa kumiliki mpira huku Ghana wakijibu haraka na kushinda mipira ya nyuma. “Katika kipindi cha kwanza timu ilijipanga ili wakipoteza mpira waweze kuuchukua katika nafasi yao”

Kipindi cha pili Brazil hawakuweza kuja na kiwango chao kama cha kwanza na kocha huyo aliamini isingewezekana kufanya hivyo. Alisema kipindi cha kwanza timu ilifanya kila kitu lakini kipindi cha pili Ghana ilikuja tofauti na pia hawakuweza kuwafungua kwani walikuwa na ukuta wa watu watano.

Kwahiyo timu iliweza kufanya vizuri katika hatua hizi tofauti lakini kuwa sawa na kile tulichofanya katika kipindi cha kwanza haifanyi kazi kila wakati. Brazil itamenyana na Tunisia siku ya Jumanne katika mchezo wao wa mwisho kabla ya kombe la Dunia nchini Qatar Novemba.

 

Brazil Yamvutia Tite

 

 

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa