Timu ya taifa ya Uingereza yashuka daraja katika michuano ya ulaya ya Uefa Nations League baada ya kupoteza mchezo wao dhidi ya timu ya taifa ya Italia uliopigwa usiku wa kuamkia leo kwa goli moja kwa bila goli pekee likifungwa na Giocomo Raspadori.

Timu hiyo imefikia hatua ya kushushwa daraja baada ya kua na matokeo mabaya katika michuano hiyo baada ya kucheza michezo mitano katika kundi lake namba tatu na kushindwa kushinda mchezo hata mmoja huku wakipoteza michezo mitatu na kusuluhu miwili.

Timu

 

 

Uingereza wataanzia hatua ya awali katika michuano inayofata ya michuano ya Uefa Nations League baada ya kutoka kwenye za daraja A na kushuka timu za daraja B kutokana na matokeo mabaya waliyovuna  katika michuano hiyo msimu huu.

Vijana hao wa Southgate wanashika mkia katika kundi la tatu wakiwa na alama zao mbili,Huku lawama nyingi zikitupwa kwa kocha wa timu hiyo kwa kushindwa kutumia ubora wa wachezaji waliopo kwenye kikosi hicho.

Mashabiki wengi wa timu hiyo wameonesha kua na wasiwasi na kiwango kinachooneshwa na timu hiyo wakati huu zikiwa zimebaki siku chache kuelekea michuano ya kombe la dunia nchini Qatar.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa