KMC: Ligi kuu ya NBC Tanzania Bara ipo kwenye moto wake, ikiwa kila timu imecheza takriban michezo 13 isipokuwa Yanga wenye michezo 12 mpaka sasa.

Ikiwa inaelekea ukingoni mwa mzunguko wa kwanza, timu nyingi zimekumbwa na majeruhi ya baadhi ya nyota wao tegemezi, mfano Simba mpaka sasa Nelson Okwa na Peter Banda wanauguza majeruhi. Ndivyo unavyoweza kusema hali kama hiyo imetajwa kukitesa kikosi cha KMC chini ya Kocha wake mkuu Thiery Hitimana.
Matokeo ya mchezo wa jana dhidi ya Tanzania Prisons yaliyomalizika kwa sare ya kutofungana, Hitimana alisema kuwa tatizo la majeruhi limechangia timu yake ya KMC kutopata matokeo ya alama 3 ambayo walikuwa wanayahitaji ili kusogea nafasi za juu zaidi kwenye msimamo.

“Timu ndogo kama ya KMC ikiwakosa wachezaji wake watano kwa sababu ya majeruhi inakuwa sio rahisi kupata matokeo, lakini ndio hivyo imebidi tuwapatie nafasi wengine”.
“Hizi timu zetu ndogo unapokuwa na kikosi kipana ila sio cha quality kubwa ni ya kawaida sana, hivyo ukiwakosa hata wachezaji wawili inakuwa ngumu kupata matokeo” Aliongea Kocha Hitimana.
Mchezo wa jana kwa KMC uliwakosa nyota wake baadhi wa kikosi cha kwanza ambao wamekuwa na mchango mkubwa sana kwa timu kama vile Emmanuel Manu, Awesu Awesu wote ni kutokana na kusumbuliwa na majeruhi.

KMC wanasalia kwenye nafasi ya 10 kwa alama 15 wakifuatiwa na Tanzania Prisons walio nafasi 11 kwa alama 15 ila utofauti ni magoli ya kufunga na kufungwa.
Beti mechi zijazo za Ligi kuu ya NBC na kombe la dunia na nyingine kupitia Meridianbet, beti na kitochi bila bando, kwenye machaguo spesho ya kombe la dunia yenye ODDS kubwa na bomba, na kama sio mpenzi wa mpira kuna michezo ya kasino mtandaoni napo unaweza kushinda jakipoti kubwa. Beti hapa.
Je wewe hucheza Kasino Mtandaoni na umekuwa ukijiuliza ni mchezo gani rahisi na mzuri kwa ushindi? Basi Usihangaike Aviator ni rahisi zaidi kucheza na kushinda, kingine cha zaidi ni kwamba Aviator Bonanza imerudi tena Cheza zaidi ujiweke kwenye nafasi ya kushinda Samsung A23.


