Klabu ya Simba inatarajia kucheza mchezo wao wa kukamilisha ratiba ya michuano ya Mapinduzi leo baada ya kuvuliwa ubingwa kwenye mchezo wake wa kwanza kwa kuchapwa bao 1-0.

Simba ilichapwa bao hilo katika kipindi cha pili dakika ya 75 na timu ya Mlandege FC na kushindwa kusawazisha bao hilo mpaka mpira kumalizika na kuwafanya washikilie mkia kwenye kundi.
Mlandege ndiye kinara wa kundi hilo akiwa na alama 4 baada ya kutoa sare mchezo wao wa kwanza na kuja kujipatia pointi kwa Mnyama dakika za jioni za mchezo huku Wekundu hao wakiwaweka wachezaji wao ambao mara nyingi huwa hawaanzi.
Leo hii ni mchezo wa kukamilisha ratiba kwani kwenye kila kundi inapita timu moja, hivyo hata Simba akishinda mechi hii ya leo bado atarejea nyumbani kutokana na kuwa mwenye pointi nyingi ndiye anayesonga mbele.

Hapa inaangaliwa je Mnyama mwenye kocha wa Kibrazil watarudi Dar es salaam patupu? bila kushinda hata mchezo mmoja?. Mchezo wa leo watamenyaana dhidi ya KVZ.

