Klabu ya Ihefu FC imeachana na wachezaji wao watano baada ya dirisha dogo la usajili kufunguliwa siku chache zilizopita.

Wachezaji hao walioachwa na klabu ni pamoja na Joseph Kinyozi, Omary, Mujwahuki, Sadoki na Oviedo ambao klabu imeona hawapo kwenye mpango wao hivyo ni vyema kuachana nao.
Taarifa hiyo imetoka kupitia ukurasa wao wa Instagram wakiwashukuru kwa kipindi chote ambacho walikuwepo klabuni hapo huku ligi ikiwa imesimama kupisha Michuano ya mapinduzi kuendelea.

Timu hiyo ipo nafasi ya 13, baada ya kucheza michezo 19, na kujivunia pointi zao 20 wakiwa wameshinda mechi mbili mfululizo. Mechi inayofuata watacheza dhidi ya Yanga kwa Mkapa.

