Winga wa klabu ya Manchester United raia wa kimataifa wa Brazil Antony Santos amerejea mazoezini ndani ya klabu hiyo baada ya kukosekana dhidi ya Bournamouth.
Winga Antony aliesajiliwa katika klabu hiyo kwa thamani kubwa zaidi alikosekana katika mchezo wa ligi kuu ya Uingereza dhidi ya klabu ya Bournamouth siku ya jumanne, Huku kocha wa klabu hiyo Erik Ten Hag akieleza winga huyo alikua anasumbulliwa na majeraha.
Klabu ya Manchester United itakua na mchezo wa kombe la Fa siku ya ijumaa dhidi ya klabu ya Everton katika dimba la Old Trafford, Huku winga huyo akitarajiwa kuwepo fiti na kucheza mchezo huo baada ya kupona majeraha yake.
Mchezaji Antony ambaye goli lake la mwisho katika ligi kuu ya Uingereza alifunga dhidi ya klabu ya Everton, Hivo winga huyo ana matumaini ya kuwepo katika mchezo huo siku ya Ijumaa kupambana na vijana wa Frank Lampard.
Klabu ya Manchester United imekabiliwa na majeruhi mwingine kwenye kikosi chake katika mchezo wa jumanne dhidi ya Bournamouth, Ambapo kiungo wake Donny Van De Beek alipata majeraha ya goti huku ikiwa haijafahamika atakua nje ya uwanja kwa muda gani.

