Kocha wa klabu ya Benfica Roger Schmidt anadai kiungo wa timu hiyo Enzo Fernandez ambaye anafukuziwa na vilabu mbalimbali barani ulaya atasalia ndani ya klabu hiyo.
Kiungo Enzo Fernandez anafukuziwa sana na vilabu vikubwa barani ulaya ambavyo vinataka saini yake, Klabu ya Chelsea ipo mstari wa mbele kufukuzia saini ya kiungo huyo fundi wa kimataifa wa Argentina lakini kocha huyo ana matumaini kibao kiungo huyo kusalia ndani ya timu hiyo.
Kocha Roger anasema “Nina matumaini Enzo atasalia hapa na sisi, Ndio Namuona akiwa na furaha na hali nzuri hapa, Sitarajii kuona mchezaji wetu yeyote wa kikosi cha kwanza akiondoka ndani ya klabu kwenye kipindi hichi” Alieleza kocha huyo akimuongelea kiungo huyo
Kiungo Enzo Fernandez mchezaji bora kijana wa michuano ya kombe la dunia amekua kwenye kipindi bora ndani ya klabu ya Benfica, Lakini vilabu vikubwa barani ulaya imekua vikihitaji saini yake kutokana na ubora ambao amekua akionesha ndani ya kombe la dunia pamoja na klabu yake.
Taarifa zibnaeleza kua klabu ya Chelsea bado haijakata tamaa juu ya kumpata kiungo Enzo Fernandez baada ya ofa yao ya awali kupigwa chini na klabu ya Benfica, Wakati huohuo taarifa za ndani kutoka klabu ya Benfica inaelezwa kiungo huyo anahitaji kuondoka ndani ya timu hiyo na kuelekea klabu ya Chelsea.

