Bondia ambaye anazidi kujizolea umaarufu kila siku Karim Mandonga amesema kuwa yeye ndiye kitambulisho cha Taifa la Tanzania kupitia kipindi cha recap kinachofanywa na EL Mando.

Mandonga ameeleza kuwa yeye ndio kipenzi cha Warembo Tanzania kwa sasa, hakuna mtu anayependwa na warembo kama yeye. Lakini mbali na hilo bondia huyo ameongeza kuwa akifika sehemu hana haja ya kuuliza mara mbili.
Hata ukienda sehemu ukitaja jina lake moja kwa moja watu watajua anatoka Tanzania, hivyo umaarufu huo unamfanya kupiga dili mbalimbali na kuhamasisha watui wengi kuingia kwenye ngumi.

Bondia huyo amevuka mipaka sio hapa Tanzania tuu bali hata nchi ya jirani Kenya mabapo alipigana pigano lake siku si nyingi watu wamezidi kumfahamu na kumfatilia kwa ukaribu kabisa.

