Beki wa kati wa Simba Henock Inonga Baka ‘Varane’ ameonekana akizidi kuimarika kwenye viwanja vya mazoezi Bunju jijini Dar es Salaam.

Beki huyo kwa muda mrefu alikuwa majeruhi na amekosekana kwenye michezo kadhaa ya Simba akiwa sambamba na baadhi ya mastaa wengine kama kiungo Mmalawi, Peter Banda na mshambuliaji Mzambia Moses Phiri.
Meneja wa Kitengo cha Mawasiliano na Habari, Ahmed Ally amewaambia wanamsimbazi kuwa ”Sasa Inonga amepona.”

Beki huyo aliumia toka mechi ambayo Simba walikuwa Kagera Kaitaba kukiwasha dhidi ya Kagera Sugar kwenye mchjezo ambao ulimalizika kwa Msimbazi kulazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 dhidi ya Wanankurukumbi.
Simba inatarajia kushuka kesho dimbani dhidi ya Singida Big Stars ambapo mechi ya kwanza kumenyana walitoshana nguvu.

