Inonga Arejea Mazoezini Simba

Beki wa klabu ya Simba Henock Inonga ambaye alipata majeraha katika mchezo wa ligi kuu ya NBC dhidi ya klabu ya Mbeya City na kumfanya kukaa nje ya uwanja kwa kipindi fulani sasa amerejea mazoezini rasmi.

Beki huyo amerudisha matumaini kwa mashabiki wa Simba kutokana na kurejea kwa beki huyo kutokana na umuhimu wake ndani ya kikosi cha Simba. Inonga ameanza mazoezi na wenzake ndani ya kikosi cha Simba kwa mara ya kwanza leo.simbaHenock Inonga amekaa nje ya timu kwa takribani wiki mbili sasa baada ya kupata majeraha katika mchezo dhidi ya Mbeya City, Taarifa za awali zilieleza kua huenda beki huyo angekaa nje ya uwanja kwa muda mrefu lakini imekua tofauti kidogo kwani ameweza kurejea ndani ya muda mfupi.

Kurejea kwa beki huyo sasa kunaiweka klabu ya Simba kwenye mikono salama katika safu ya ulinzi ya klabu hiyo, Safu ya ulinzi ya klabu ya Simba ilionekana kutetereka katika michezo miwili iliyocheza bila ya kua na beki huyo mwenye ubora mkubwa.simbaBeki Henock Inonga baada ya kurejea mazoezini rasmi ndani ya klabu ya Simba sasa anatarajiwa kuwepo katika michezo ya ligi kuu ya NBC pamoja na michuano mingine, Klabu ya Simba inajiandaa na michuano mbalimbali ikiwemo NBC, FA, na ligi ya mabingwa Afrika hivo wanahitaji kua na wachezaji wao muhimu na beki huyo ni miongoni mwao.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.