Mbappe Anaamini Wanaweza Kupindua Meza Dhidi ya Bayern

Staa wa klabu ya PSG Kylian Mbappe amesema anaamini kua klabu yake inaweza kupindua meza katika mchezo wa pili wa ligi ya mabingwa ulaya baada ya kupoteza mchezo wa jana nyumbani.

Klabu ya PSG jana ilipoteza mchezo wao wa kwanza wa ligi ya mabingwa ulaya hatua ya 16 bora wakiwa katika dimba lao la nyumbani kwa bao moja kwa bila, Lakini nyota wa klabu hiyo Mbappe anaona bado wana nafasi ya kupindua meza na kuweza kufuzu hatua inayofuata.MbappeMchezo wa marudiano kati ya klabu ya PSG dhidi ya Bayern Munich utapigwa wiki mbili mbele katika dimba la Allianz Arena baada ya mchezo wa jana kupigwa katika dimba la Parc de Princes na Bayern kuibuka na ushindi katika mchezo huo, Lakini mchezo wa pili unatarajiwa kua na ushindani zaidi kwani hakuna timu iliyojihakikishia kupata matokeo.

Mchezaji Mbappe anasema wanakwenda katika dimba la Allianz Arena kuhakikisha wanafuzu hatua inayofuata, Kwani hakuna goli la ugenini siku hizi hivo wanachohitaji ni kufunga mabao katika mchezo wao dhidi ya Bayern ili kuweka ubao sawa na hatimae kupindua meza kabisa na kufuzu hatua ya robo fainali.MbappeKatika hali ambayo sio ya kawaida mchezaji Mbappe ambaye ilielezwa ataukosa mchezo huu lakini alionekana katika mchezo dhidi ya Bayern, Huku mchezaji mwenyewe akithibitisha kua hakutakiwa kucheza mchezo huo lakini akisema alitaka kucheza mchezo huo ili kuisaidia timu yake pamoja na wachezaji wenzake.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.