Cancelo: Sijagombana na Guardiola

Beki wa klabu ya Manchester City Joao Cancelo anayekipiga klabu ya Bayern Munich kwa mkopo amekanusha taarifa zinazotolewa kua aligombana na kocha Pep Guardiola na ndio sababu ya kuondoka klabuni hapo.

Beki Joao Cancelo ameondoka ndani ya klabu ya Manchester City kwenye dirisha dogo la mwezi Januari ukiwa usajili wa kushtukiza zaidi, Hivo kupelekea kuzuka kwa maneno mbalimbali kua mchezaji huyo amegombana na Pep Guardiola na kitu ambacho mchezaji huyo amekikanusha na kusema kocha huyo na klabu walimpa kila kitu.canceloBeki huyo alijikuta anakosa nafasi katika baadhi ya michezo ndani ya klabu hiyo na kuelezwa kua mchezaji huyo alipishana na kocha wake, Lakini beki huyo amesema jambo hilo sio la kweli na ni uzushi na kusisitiza anamshukuru kocha Guardiola katika maisha yake ya soka.

Beki Cancelo alizungumza baada ya ushindi wa bao moja kwa bila walioupata Bayern Munich katika mchezo wa jana usiku na kusema “Watu wanaosema nilipigana na Guardiola sio kwelii ni uongo. Sikujiskia muhimu kwa michezo iliyopita. Nilizungumza na kocha na alikubali pia na kwa pamoja na klabu tukakubaliana ilipaswa mimi kuondoka kwakua ilikua bora kwangu”canceloMkataba wa Cancelo ndani ya Manchester City utafikia ukomo Juni 2027 hivo ana uwezekano wa kuendelea kuitumikia klabu hiyo kutoka jijini Manchester, Huku yeye mwenyewe akithibisha bado ana nafasi ya kurudi ndani ya klabu ya Manchester City.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.