Xavi: Tunataka Kuonesha Ubora Wetu Dhidi ya Man United

Kocha wa klabu ya Fc Barcelona Xavi Hernandez amesema klabu yake imedhamiria kuonesha kua ina uwezo na ubora wa kushindana kupitia mchezo wa kombe la Europe League dhidi ya klabu ya Manchester United.

Klabu ya Barcelona itashuka dimbani kumenyana na Manchester United katika mchezo wa mtoano wa kombe la Europe League utakaopigwa katika dimba la Camp Nou hapo kesho, Kocha Xavi ambaye ameirudisha klabu hiyo kwenye nyakati nzuri na kuweka wazi kua klabu yake iko tayari kuonesha inao uwezo wa kushindana dhidi ya United.xaviKlabu ya Barcelona haijapoteza michezo 16 tangu walipopoteza dhidi ya Barcelona kwa mabao matatu kwa bila dhidi ya Bayern Munich, Kuanzia hapo klabu hiyo imefanikiwa kupata matokeo katika michezo 11 huku ikitoka sare katika michezo mitano kati ya 16 iliyopita na hii inaonesha namna klabu hiyo imeimarika kwa kiwango kikubwa.

“Kesho ni mechi kubwa, Timu zote mbili zimefika wakati mzuri katika msimu, Ten Hag amebadilisha taswira ya timu japo haikua rahisi kwao, Lakini wanafanya kazi kubwa”  maneno ya kocha Xavi akionesha namna anafurahishwa na mchezo huo lakini akimsifu kocha wa klabu ya Man United kutokana na kazi anayoifanya ndani ya klabu hiyo.xaviKocha Xavi ameendelea kusisitiza kesho ni siku ya kuonesha wao wana ubora mbele ya moja ya timu bora kwenye michuano hiyo, Lakini akieleza wazi anatambua Man United hawapo kwenye ubora wao waliokua nao kipindi cha nyuma lakini wana wachezaji ambao wapo kwenye wakati mzuri sana hivo anatarajia mchezo mzuri sana.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.