Klabu ya Yanga inatarajiwa kushuka dimbani hii leo kusaka pointi tatu dhidi ya Geita Gold ya Geita ambayo ipo nafasi ya tano kwenye msimamo wa ligi.

Mchezo huo atapigwa Chamazi Complex majira ya saa 12:15 jioni huku Yanga wakiwa bado ni vinara wa ligi wakiwa na pointi zao 62 mbele ya pointi tano kwa anayemfuata wa pili.
Pia vijana hao wa Nasredine Nabi wameshinda mechi 10 mfululizo kwenye ligi huku mechi ya leo endapo wakishinda itakuwa ya 11 wakati Geita ya Minziro wao mechi iliyopita wametoka kupoteza.
Tofauti ya pointi yao kati ya hizi timu mbili ni 28. Je nani kuondoka na ushindi hii leo huku mechi ya mwisho walipokutana Young Africans aliondoka na ushindi akiwa ugenini.

Ikumbukwe kuwa Mabingwa hawa wa kihistoria wanafukuzia ubingwa wa pili mfululizo kwenye ligi tena baada ya msimu uliopita kuchukua na sasa wanafaida ya pointi tano mbele hivyo huenda wakafaidika na hilo.

