Winga wa klabu ya Manchester United Mason Greenwood ambaye amekua nje ya uwanja kwa muda wa takribani mwaka mmoja na miezi mitatu anafanya mazungumzo na klabu yake hiyo ili kuangalia urejeo wake.
Winga Greenwood ambaye alikamatwa Januari 31 2022 alikamatwa kwa tuhuma za makosa ya ubakaji na unyanyasaji wa kingono dhidi ya mpenzi wake, Lakini mahakama jijini Manchester ilithibitisha winga huyo hana hatia juu ya tuhuma hizo na kuachiwa huru.
Winga huyo wa kimataifa wa Uingereza anafanya mazungumzo na klabu yake kwasasa kuangalia uwezekano wa kurejea katika timu hiyo haraka iwezekanavyo, Ni wazi kua mchezaji huyo anataka kusalia ndani ya klabu hiyo na kuendelea kuitumikia na sasa anasubiria maamuzi ya klabu yake.
Kocha Erik Ten Hag inaelezwa anavutiwa na kipaji cha kijana Mason Greenwood hivo anatamani mchezaji huyo aendelee kuitumikia klabu hiyo kwasababu anakiona kipaji kikubwa ndani ya mchezaji huyo, Hivo maamuzi ya mchezaji huyo kurejea klabuni hapo ndio yanasubiriwa.
Kocha Ten Hag inaelezwa kua anataka mchezaji Greenwood aungane na timu hiyo mwishoni mwa msimu wakiwa wanajiandaa na msimu ujao, Hivo inawezekana winga huyo akarejea kwenye timu hiyo kutokana na kocha Ten Hag inaelezwa anakubali uwezo wa mchezaji huyo kwa kiwango kikubwa.

