Nini Hatma ya KMC Ligi Kuu?

Klabu ya KMC inatarajiwa kumenyana dhidi ya Tanzania Prisons hii leo huku timu hiyo ikipigania kutoshuka daraja msimu huu.

 

Nini Hatma ya KMC Ligi Kuu?

KMC inashikilia nafasi ya 13 kwenye msimamo wa ligi kuu baada ya kucheza michezo yapo 28, huku wakiwa wameshinda mechi zao 7, sare 8 na kupoteza mechi zao 13 hadi sasa wakikusanya pointi zao 29.

Wakati kwa upande wa Tanzania Prisons wao wanashikilia nafasi ya 8, wakiwa wameshinda mechi zao 9, sare 7, na kupoteza mara 12 kwenye michezo yao 28 waliyocheza.

Nini Hatma ya KMC Ligi Kuu?

Kwenye mchezo wa mkondo wa kwanza hakuna aliyekuwa mbabe kati yao huku mwenyeji akiwa na mwendelezo mzuri wa matokeo baada ya kushinda mechi zake 4 mfululizo. Wakati mgeni yeye kwenye mechi zake tano ameshinda mbili pekee na kupoteza tatu.

KMC anahitaji ushindi mechi hii, kwani mchezo wa mwisho atakipiga dhidi ya Mbeya City ambaye naye pia anahitaji ushindi kwa namna yoyote ili abaki ligi kuu. Je nini hatma ya Walipa Kodi?

 

 

 

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.