Je Simba Kumshusha Daraja Polisi Tanzania Leo?

Ligi kuu ya soka Tanzania bara inaendelea hii leo huku michezo yote ya raundi ya 29 kupigwa leo, ambapo mchezo wa saa 12:00 ni kati ya Simba dhidi ya Polisi Tanzania katika dimba la Chamazi.

 

Je Simba Kumshusha Daraja Polisi Tanzania Leo?

Simba yupo nafasi ya pili akiwa na pointi zake 67 huku Polisi Tanzania wao wapo nafasi ya 15 wakiwa na pointi zao 25 na hatma yao ipo mbele ya mnyama ambaye msimu huu hajaambulia chochote.

Polisi Tanzania walishindwa kushuka daraja kwenye mechi yao iliyopita kutokana na ushindi ambao waliupata na hivyo kuendelea kusalia kwenye ligi huku Ruvu Shooting yeye akienda ligi daraja la kwanza.

Je Simba Kumshusha Daraja Polisi Tanzania Leo?

Simba kupitia kocha wao msaidizi Jumma Mgunda amesema kuwa, matarajio yao kwenye mchezo huo ni kupata ushindi ili wamalize ligi kwa kushinda mechi zao lkaini anaamini kuwa watapata upinzani kutoka kwa Maafande.

 

 

 

 

Acha ujumbe