Klabu ya Man United yafanikiwa kumalizana na klabu ya Inter Milan kwajili ya kumnunua golikipa wa timu hiyo Andre Onana kwa ada ya uhamisho ya Euro milioni 48.
Man United walishamalizana na golikipa huyo kwenye maslahi binafsi wiki kadhaa nyuma lakini suala lililosubiriwa ni klabu hiyo kutuma ofa itakayokubaliwa na klabu ya Inter Milan ambapo mpaka sasa asilimia 99 dili hilo limekamilika.
Klabu ya Inter Milan ilikataa ofa tatu za klabu ya United ambazo walizituma kwa klabu hiyo kutoka nchini Italia, Lakini ofa ya mwisho ya mashetani hao wekundu imekubaliwa na mchezaji huyo ataelekea jijini Manchester.
Man United imehakikisha inapata huduma ya golikipa huyo wa kimataifa wa Cameron, Kwani aliyekua golikipa wa klabu hiyo David De Gea ametimka ndani ya timu hiyo baada ya mkataba wake kumalizika.
Andre Onana amekua kwenye kiwango bora sana ndani ya klabu ya Inter Milan jambo ambalo liliwavutia Man United kuhitaji saini yake, Huku ikiwa ni chaguo zaidi la kocha Ten Hag ambaye alishawahi kufanya kazi na mchezaji huyo ndani ya klabu ya Ajax.

