Jesus Apata Majeraha Tena

Mshambuliaji wa klabu ya Arsenal raia wa kimataifa wa Brazil Gabriel Jesus imearifiwa amepata majeraha ya goti hatakuepo kwenye mchezo wa Arsenal dhidi ya Monaco usiku wa leo.

Mshambuliaji Jesus amekua akiandamwa na majeraha mara kwa mara tangu ajiunge na klabu hiyo akitokea klabu ya Manchester City ambapo mwaka jana kipindi cha kombe la dunia alipata majeraha ambayo yalimueka nje ya uwanja kwa muda mrefu.JesusKlabu ya Arsenal yenyewe ndio taarifa ya majeraha ya mshambuliaji wake huyo kuelekea mchezo wao wa fainali wa kombe la Emirates ambapo watakipiga na Monaco na mshambuliaji huyo atakosekana katika mchezo huo.

Klabu ya Arsenal imesema itatoa taarifa zaidi baadae juu ya majeraha aliyoyapata mchezaji huyo na taarifa hiyo ikiwa inatizamia zaidi kutoa taarifa ya muda gani mchezaji huyo atakaa nje ya uwanja baada ya jopo la madaktari kutoa taarifa.JesusMshambuliaji Jesus licha ya majeraha ambayo amekua akiandamwa nayo mara kwa mara ndani ya kikosi cha Arsenal, Lakini amekua kwenye kiwango bora pale ambapo anakua yupo fiti hivo nipigo kubwa kwa klabu hiyo.

 

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.