West Ham Hawajasajili Mpaka Sasa

Klabu ya West Ham mpaka sasa ndio klabu pekee ambayo haijafanya usajili wowote kwenye dirisha hili kubwa mpaka sasa kuelekea msimu mpya wa ligi kuu ya Uingereza.

Klabu zinazoshiriki ligi kuu ya Uingereza msimu ujao zimeelezwa kufanya usajili mpaka sasa angalau wa mchezaji mmoja, Lakini West Ham pekee mpaka sasa ndio hawajaripotiwa kufanya usajili wa aina yeyote.west hamKikosi hicho cha kocha David Moyes ambacho kilifanikiwa kutwaa taji la la michuano ya Uefa Conference league, Wameanza kutia mashaka juu ya hali yao msimu ujao kama mpaka dirisha litafungwa hawajafanya usajili wowote.

Kitu kinachoshtua kuhusiana na wagonga nyundo hao kutoka jiji la London ni wao kuachia baadhi ya wachezaji wao na wengine ni muhimu sana, Klabu hiyo imemuuza kiungo wao ambaye pia alikua nahodha wa timu Declan Rice na mpaka sasa hawapata mbadala wake.west hamKlabu ya West Ham ilifanikiwa kua na msimu mzuri wa 2022/23 lakini wanatia mashaka mpaka sasa kutokana na kinachoendelea, Kwani wameachia wachezaji muhimu kwenye timu na hawajafanikiwa kusajili mchezaji yeyote.

Acha ujumbe