Golikipa gwiji raia wa kimataifa wa Italia Gianluigi Buffon ametangaza kuachana na soka rasmi leo akiwa anaitumikia klabu yake ya Utotoni ya Parma.

Buffon amestaafu kucheza soka la ushindani leo kama moja ya magolikipa wenye heshima kubwa sana katika mchezo wa soka duniani kwani ameacha alama kubwa kwenye mchezo huo pendwa zaidi duniani.BuffonGolikipa huyo mkongwe amekua kwenye kiwango bora tangu akiwa klabu ya Parma ambapo ndiyo iliyomkuza kabla ya kujiunga na klabu ya Juventus mwaka 2001 ambapo amepata mafanikio makubwa na klabu hiyo.

Golikipa huyo wa kimataifa wa Italia alifanikiwa kushinda kila taji alilolishindania akiwa na klabu ya Juventus, Huku akikosa taji la ligi ya mabingwa ulaya tu ambapo amefanikiwa kucheza fainali tatu za michuano hiyo.BuffonGolikipa Gianluigi Buffon dunia inamtambua kama moja ya golikipa bora kuwahi kuubariki mpira wa miguu, Huku akikumbukwa zaidi kwa kiwango bora alichokionesha kwenye michuano ya kombe la dunia mwaka 2006 ambapo timu yake ya taifa ya Italia ilitwaa ubingwa.


JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa