Tottenham Kushusha Beki Mpya Kutoka Ujerumani

Klabu ya Tottenham Hotspurs ipo mbioni kumalizana na klabu ya Wolfsburg ya nchini Ujerumani kwajili ya kupata saini ya beki wa klabu hiyo Micky van de Ven.

Klabu ya Tottenham imefanikiwa kufikia makubaliano na klabu ya Wolfsburg kwa kutoa kiasi cha euro milioni 50 ambayo itajumuisha na bonasi katika kuhakikisha wanapata saini ya beki huyo.TottenhamVijogoo hao kutoka jiji la London wako kwenye harakati za kuitengeneza klabu hiyo na kuhakikisha wanairudisha kwenye ubora ambao wameupoteza kwa misimu kadhaa haswa msimu uliomalizika.

Beki huyo mwenye umri wa miaka 22 amekua kwenye kiwango kizuri ndani ya klabu hiyo nchini Ujerumani ikiwa ni sababu kubwa iliyopelekea Spurs kuvutiwa na umahiri wa beki huyo wa kimataifa wa Uholanzi.TottenhamTottenham wanataka kutengeneza safu ngumu ya ulinzi ambao itakua ikiundwa na beki Cristian Romero ambaye ataungana na Micky van de Ven, Hivo kuelekea msimu ujao ni wazi Spurs msimu ujao wanaweza kurejea kwenye ubora wao.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.