West Ham wanapanga kumnunua kiungo wa Ajax Mohammed Kudus endapo nyota wao wa Brazil Lucas Paqueta akiondoka kwenda Manchester City ambao wamepanga dau lingine kwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25.

Ripoti ya talkSPORT inadai kuwa klabu hiyo haina nia ya kumtoa mchezaji mwingine bora msimu huu lakini haitasimama katika njia ya Paqueta iwapo mabingwa hao wa Ligi watafikia hesabu yao.
Odds kubwa kasino ya mtandaoni na michezo ya sloti ni vitu vinavyoweza kubadilisha maisha yako kwa kukupatia pesa nyingi. Ingia mchezoni hapa.
Kisha wanaweza kuwekeza tena fedha hizo kwa Kudus, ambaye atajiunga na nyongeza mpya Edson Alvarez na James Ward-Prowse huko London Mashariki West ham

Brighton pia wana nia thabiti ya Kudus na inasemekana kuwa alikuwa na ofa iliyokubaliwa kwa mchezaji huyo wa kimataifa wa Ghana lakini hawakuweza kukubaliana na masharti ya kibinafsi.
Aviator, poker, Roullette, Wild Icy Fruits, Piggy Party na mingine kibao upige pesa na Meridianbet. Ingia www. meridianbet.co.tz.

Kudus mwenye miaka 23, alianza kampeni yake ya Eredivisie kwa bao katika ushindi wa 4-1 wa Ajax dhidi ya Heracles Jumamosi na ana uwezo wa kucheza winga au kupitia katikati.
Ana mchango wa mabao 25 katika mechi 64 za ligi kwa wababe hao wa Uholanzi.

