Onana aanza vizuri Man United

Kipa wa klabu ya Manchester United raia wa kimataifa wa Cameroon Andre Onana amefanikiwa kuanza vizuri ndani ya kikosi cha Manchester United katika mchezo wa kwanza wa ligi kuu ya Uingereza.

Katika mchezo wa jana wa kwanza kwa klabu ya Manchester United katika kigi kuu ya Uingereza golikipa Onana alikua kwenye kiwango bora akifanikiwa kuchomoa michomo kadhaa ambayo iliifanya klabu hiyo kupata alama tatu.onanaManchester United imefanikiwa kupata ushindi wa bao moja kwa bila jana dhidi ya klabu ya Wolverhampton, Huku kiwango kikubwa ndani ya timu hiyo kikioneshwa na golikipa huyo wa zamani wa klabu ya Inter Milan ya Italia.

Kudhihirisha kua Onana alikua kwenye ubora mkubwa sana usiku wa jana alifanikiwa kuibuka nyota wa mchezo katika mchezo dhidi ya Wolverhampton na kuondoka katika mchezo huo bila kuruhusu bao lolote.onanaManchester United licha ya kupata ushindi katika mchezo wa jana lakini walionesha kiwango cha chini sana,Kitu ambacho kimefanya mpaka golikipa kuibuka kama nyota wa mchezo kwani wachezaji wa ndani kwa kiwango kikubwa walikosa utulivu,umakini, na hali ya kujiamini.

Acha ujumbe