Bado ni kizungumkuti kwenye sakata la kiungo wa Simba Yusuph Kagoma, baada ya klabu ya Yanga kumshitaki mchezaji huyo kwenye Kamati ya Maadili na Hadhi ya Wachezaji iliyopo chini ya TFF.

Yanga wanadai mchezaji huyo alivuta mkwanja wa usajili na kusaini karatasi za awali za kukubali kuichezea Yanga, na wakati wakisubiri taratibu zote kukamilika wakashangaa nyota huyo aliyekuwa mali ya Fountain Gate FC ametambulishwa na Simba.
Sasa Meridian Sports imeingia chimbo kusaka ukweli na undani wa sakata hilo, na imefanikiwa kupata ripoti kamili ya nini chanzo cha matatizo.
Mtoa taarifa huyo ambaye aliwahi kuwa kiongozi Singida Fountain Gate FC, amesema, Kagoma mwenyewe ndiye aliyejichanganya, kwa kuwa alishakubali kuitumikia Yanga na kuchukua kiasi cha fedha, huku uongozi wa Fountain Gate ukiwa pia umekubaliana dili ya Kagoma kwenda Yanga.


