ISHU YA KAGOMA UKWELI NI HUU

Bado ni kizungumkuti kwenye sakata la kiungo wa Simba Yusuph Kagoma, baada ya klabu ya Yanga kumshitaki mchezaji  huyo kwenye Kamati ya Maadili na Hadhi ya Wachezaji iliyopo chini ya TFF.

ISHU YA KAGOMA UKWELI NI HUU

Yanga wanadai mchezaji huyo alivuta mkwanja wa usajili na kusaini karatasi za awali za kukubali kuichezea Yanga, na wakati wakisubiri taratibu zote kukamilika wakashangaa nyota huyo aliyekuwa mali ya Fountain Gate FC ametambulishwa na Simba.

Sasa Meridian Sports imeingia chimbo kusaka ukweli na undani wa sakata hilo, na imefanikiwa kupata ripoti kamili ya nini chanzo cha matatizo.

Mtoa taarifa huyo ambaye aliwahi kuwa kiongozi Singida Fountain Gate  FC, amesema, Kagoma mwenyewe ndiye aliyejichanganya, kwa kuwa alishakubali kuitumikia Yanga na  kuchukua kiasi cha fedha, huku uongozi wa Fountain Gate ukiwa pia umekubaliana dili ya Kagoma kwenda Yanga.

ISHU YA KAGOMA UKWELI NI HUU

Lakini, baadae mchezaji akapokea ofa kutoka Simba ambayo ilikuwa ni kubwa Zaidi ya ile ya Yanga, kiasi ambacho mchezaji akashawishika kuchukua mpunga huo na kusaini mkataba, na kuufanya sasa mfuko wake kutana kwa hela aliyopewa Yanga na ile ya Simba.

Fountain Gate walipotafutwa na Simba, ikabidi warudi kwa mchezaji kujua wapi anataka kuelekea, ndipo Simba na Fountain wakamalizana na mchezaji akauzwa akiwa na mkataba wa mwaka mmoja.

Hivyo inawezekana Yanga wakawa  na sehemu Fulani ya madai kwa Kagoma, kwa kuwa ni kweli alichukua hela za Yanga, kabla ya kusaini Simba

Acha ujumbe