FOUNTAIN GATE, KENGOLD MECHI YA KIHISTORIA

Kesho Jumatano kwenye Uwanja wa Tanzanite Kwaraa kuna mchezo wa kihistoria unakwenda kuchezwa, kati ya Fountain Gate FC ambao ni wenyeji dhidi ya Ken Gold FC kutoka Mbeya.

FOUNTAIN GATE, KENGOLD MECHI  YA KIHISTORIA

Fountain Gate watakuwa wanacheza mchezo wao wa kwanza msimu huu wakiwa nyumbani ikiwa pia ni kwa mara ya kwanza Mkoa wa Manyara na Wilaya ya Babati itakuwa inashuhudia Ligi Kuu Bara ikichezwa mbele ya macho yao.

Pia meridianbet inatoa michezo ya kasino ya mtandaoni kama vile, Aviator, poker, Roullette, sloti na mingine kibao. Ingia meridianbet na ucheze sasa.

Kocha Mkuu wa Fountain Gate Mohamed Muya amesema huu ni mchezo ambao alama zake tatu kuzipata ni muhimu Zaidi kwa kuwa ni mchezo ambao  utakuwa unatazamwa na wana Babati wengi, huku akisema kikosi chake kimefanya maandalizi ya kutosha kuelekea kwenye mchezo huo.

FOUNTAIN GATE, KENGOLD MECHI  YA KIHISTORIA

“Ni mchezo muhimu sana kwetu, kwa kuwa tunacheza nyumbani kwa  mara ya kwanza na itakuwa ni lazima kupata  ushindi kwa kuwa matumaini ya watu wa Manyara ni kuona timu inapata alama tatu,” amesema Muya.

 

Acha ujumbe