FOUNTAIN GATE NA MBUNI FC JUMAMOSI

KLABU ya Fountain Gate FC inatarajia kucheza mechi ya kirafiki na Mbuni FC tareha 7 siku ya Jumamosi kwenye Uwanja wa Tanzanite Kwaraa uliopo Babati mkoani Manyara.

Mbuni ambayo inatokea mkoani Arusha inajiandaa kucheza mechi zake za Ligi Daraja la Kwanza inayoanza mwezi wa 10.

Fountain Gate wamerejea kwenye Uwanja wa mazoezi leo Baada ya mapumziko ya siku mbili, ikiwa ni siku chache wacheze na Namungo na kuvuna alama tatu.

Fountain Gate FC wanajiandaa kucheza na Ken Gold kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara tarehe 11 kwenye Uwanja wa Tanzanite Kwaraa saa 10:15 jioni.

Acha ujumbe