SIMBA KUKIPIGA MECHI YA KIRAFIKI WIKIENDI HII

KLABU ya Simba inatarajia kucheza mechi ya kirafiki wikiendi hii kabla ya kusafiri kwenda Libya kucheza mechi ya kwanza ya Kombe la Shirikisho dhidi ya Al Tripoli.

Ahmed Ally, Afisa habari wa mawasiliano wa Simba ameiambia Meridian Sports kuwa inawezekana mchezo huo ukawa dhidi ya timu ya Ligi Kuu au Ligi Daraja la Kwanza ambapo kesho Jumatano watasema watacheza na nani.

“Tunaendelea na mazoezi kama kawaida kujiandaa na safari ya kwenda Libya kucheza mechi yetu ya kwanza ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Al Ahli Tripoli ya Libya.

“Lakini kabla ya hapo Wikiendi hii tutacheza mechi ya kirafiki na timu ambayo tutawatangazia kesho au Kesho Kutwa Jumatano,”

Acha ujumbe