Simba Yaendeleza Vichapo

Klabu ya Simba imeendelea kutoa dozi kwenye ligi kuu ya NBC baada ya kufanikiwa kutoa kipigo kizito cha mabao manne kwa bila dhidi ya klabu ya Singida Fountain Gate.

Simba wameonekana kua kwenye ubora mkubwa wakitengeneza nafasi mara kwa mara ambapo ilipelekea dakika ya 13 tu ya mchezaji Jean Charles Ahoua alipiga pasi kwa Edwin Balua ambaye aliwaandikia bao la kwanza katika mchezo huo wekundu wa msimbazi kabla ya Steven Mukwala kuandika bao la pili dakika ya 44 kuelekea mapumziko.simbaWekundu wa msimbazi walitawala zaidi kipindi cha kwanza cha mchezo huo kama ambavyo walifanya katika mchezo wao wa kwanza wa ligi kuu ya NBC dhidi ya Tabora United, Jambo ambalo liliwafanya vijana wa kocha Fadlu Davids kuweza kutengeneza nafasi nyingi za kufunga katika mchezo huo.

Kipindi cha pili kiliendelea kwa Wekundu wa msimbazi kuendelea kutawala mchezo huo kama ambavyo walifanya kipindi cha kwanza cha mchezo, Dakika nane tu zilitosha kuwafanya Simba kupata goli la tatu la mchezo dakika ya 58 kupitia kwa kiungo wao Jean Charles Ahoua.simbaKlabu ya Simba haikuridhika na mabao matatu ambapo dakika ya 84 Valentino Mashaka ambaye alitokea nje alifanikiwa kupiga msumari wa mwisho katika mchezo huo akifunga bao la nne, Wekundu wa msimbazi sasa wanakwea kileleni mwa msimamo wa ligi kuu ya NBC wakiwa ana alama zao sita katika michezo miwili.

Acha ujumbe