Ripoti kutoka Hispania zinaonyesha kuwa Carlo Ancelotti huenda akawa kocha wa Brazil kwa ajili ya mechi za kufuzu Kombe la Dunia mwezi Juni, huku Real Madrid tayari wakiwa wamempanga Xabi Alonso kutoka Bayer Leverkusen kama mrithi wake.

Kocha huyo wa Kiitaliano haitarajiwi kuendelea kuwa kwenye benchi la Real Madrid baada ya msimu huu, lakini kuna uwezekano akaondoka hata kabla ya hapo.
Pia meridianbet inatoa michezo ya kasino ya mtandaoni kama vile, Aviator, poker, Roullette, sloti na mingine kibao. Ingia meridianbet na ucheze sasa.
Kuna tetesi kuwa Ancelotti anaweza kufutwa kazi iwapo atashindwa kuifunga Barcelona kwenye fainali ya Copa del Rey wikendi hii.
Wakati huo huo, Relevo wameripoti kuwa Real Madrid hawatamweka Ancelotti kwa ajili ya kampeni ya Kombe la Dunia la Klabu litakalofanyika Marekani kuanzia Juni hadi Julai.


