Miongoni mwa hukumu zilizotolewa na vyombo vya habari vya Italia kufuatia kipigo cha 1-0 cha Milan dhidi ya Atalanta, kiwango cha Joao Felix kilikosolewa vikali. “Anaweza kurudi Chelsea kwa furaha,” waliandika baadhi ya wachambuzi.
Rossoneri wamejikuta wakishuka hadi nafasi ya tisa kwenye msimamo wa Serie A kufuatia kichapo hicho cha nyumbani.
Hii inamaanisha kwamba matumaini yao makubwa ya kucheza michuano ya Ulaya sasa yamebaki kwenye Coppa Italia, ambako watakutana na Inter katika nusu fainali siku ya kesho.
Wachezaji wote walikumbwa na ukosoaji kutoka kwa vyombo vya habari vya Italia, lakini Joao Felix alikosolewa zaidi, baada ya kuingia kama mchezaji wa akiba na kucheza dakika 15 bila kuonyesha chochote cha maana.
“Kumtumia ilikuwa hatua ya kukata tamaa na haikufanikiwa. Kamari iliyopotea anaweza kurudi alikotoka kwa furaha,” liliandika gazeti la Corriere della Sera.




